01 | Tafsir Surah Yaasin
Utangulizi 1. Majina ya Sura Yasin 2. Aya za Sura Yasin 3. Imeteremka wapi Sura Yasin? 4. Fadhila za Sura Yasin. 5. Nini lengo la Sura Yasin? 6. Nini maudhui za Sura Yasin? 7. Fasili ya aya za mwanzo za juzuu ya kwanza ya Yasin na maelezo yake.
02 | Tafsir Surah Yaasin
1. Juzuu ya kwanza ya Sura Yasin inaongelea nini? (Utume) 2. Fasili tofauti za neno Yasin. 3. Hurufu Muqattaat ni nini? 4. Nini makusudio ya hurufu Mukatwah? 5. Rai tofauti kuelezea hurufu Mukatwah na majina ya sura katka Qur’an. 6. Fasili za aya tatu za kwanza za Sura Yasin.
03 | Tafsir Surah Yaasin
1. Muhtasari mfupi wa darsa iliopita. 2. Dalili za kuthibitisha Utume. 3. Ni ipi Miujiza aliyokuja nayo Mtume Muhamad (S.A.W)? 4. Maana ya Sura Mustakeem na maelezo yake. 5. Sura Mustakiim, vikwazo wapitavyo waja na jinsi watakavoivumbua. 6. Sampuli za njia za kuutekeleza uislam.
04 | Tafsir Surah Yaasin
1. Nini yalikua malengo yakutimiliza Mitume? 2. Ni vipi mja atafikia malengo aliyoumbiwa? 3. Adhabu na maelezo yake. 4. Nini malengo ya adhabu kwa mja? 5. Mambo gani ya kuzingatia kabla na wakati mtu anapotoa adhabu kwa mja? 6. Ni makosa gani yafaa kunyamaziwa na yapi hayafai kufumbiwa macho? 7. Ni zipi athari za adhabu...
05 | Tafsir Surah Yaasin
1. Fasili ya aya ya saba ya Sura Yasin. 2. Misimamo gani iliyoletwa kwa watu wa Mitume? 3. Sura Yasin imegawa waja katika makundi mangapi? 4. Sababu zipi zawafanya waja kukubali au kuupinga Utume? 5. Sababu kwanini waja hawakuamini Mitume na Sura Mustakeem.
06 | Tafsir Surah Yaasin
1. Fakhrudin Razi azungumzia nini kuhusu njia waja wanazotumia kupata pepo za Allah katika Sura Yasin? 2. Sampuli mbili za maisha ya mja ni zipi? 3. Hatua zipi wataalam walizochukua kusoma maarifa? 4. Ni vitu gani vyaua mawasiliano kati ya waja na ulimwengu wake? 5. Nini mapungufu ya vyombo vya mawasiliano kwa mwanadamu?
07 | Tafsir Surah Yaasin
1. Fikra zinazohusika na maelezo aya 7-10 ya Sura Yasin. 2. Vyombo zipi watazitegemea kuwasiliana na ulimwengu? 3. Mja anapozaliwa huwa kama ardhi tupu hamiliki maarifa yoyote kwa mujibu wa Qur’an. 4. Hisia za mawasiliano zisipofanya kazi, ni kazi kufikisha maarifa kwa mja. 5. Hisia zipi za kwanza mja hutumia pale mwanzoni baada ya kuzaliwa?...
08 | Tafsir Surah Yaasin
1. Muendelezo wa njia zitumiwazo na waja kuwasiliana na ulimwengu na maarifa. 2. Masharti gani yafatwe ili vyombo vya mawasiliano vitumike? 3. Ni vipi watazuia vyombo vya mawasiliano visifanye kazi? 4. Ni vipi kupenda sana ulimwengu kwazuia vyombo kufanya kazi? 5. Ni vipi kibri na kujisikia vyaharibu na vyafunga vyombo vya maarifa?
09 | Tafsir Surah Yaasin
1. Ni vipi ujinga waharibu vyombo vya maarifa? 2. Ni vipi unafiki waharibu vyombo vya maarifa? 3. Ni vipi kukataa haki kwaharibu vyombo vya maarifa? 4. Ni vipi kufata kwa utu (utakatifu uliozidi) kwaharibu vyombo vya maarifa? 5. Ni vipi madhambi yaharibu vyombo vya maarifa?
10 | Tafsir Surah Yaasin
1. Maelezo ya aya ya 11 kwa ufanisi. 2. Zipi ni tiba za mambo yaharibia vyombo vya maarifa? 3. Nini maana ya wakhashia rahmaan min ghaib? 4. Tofauti ya starehe za peponi na ulimwenguni. 5. Sifa za waja ambao watamkubali Mtume ni zipi? 6. Sharti za maarifa/imani ni zipi?
11 | Tafsir Surah Yaasin
1. Maelezo ya ufanisi wa aya ya 12 kwa ufupi. 2. Misingi mitatu ya uislamu ni ipi? 3. Maelezo ya aya Maakadamu waathalaum. 4. Sifa za amali kadaamia na atharia. 5. Sampuli za vitabu viandikavyo amali za waja. 6. Maswali na majibu ya aya ya 12 ya Sura Yasin.
12 | Tafsir Surah Yaasin
1. Maelezo ya ufanisi wa aya ya 12 kwa ufupi. 2. Misingi mitatu ya uislamu ni ipi? 3. Maelezo ya aya Maakadamu waathalaum. 4. Sifa za amali kadaamia na atharia. 5. Sampuli za vitabu viandikavyo amali za waja. 6. Maswali na majibu ya aya ya 12 ya Sura Yasin.
13 | Tafsir Surah Yaasin
1. Maudhui ya juzuu ya pili ya Sura Yasin kwa ufupi. 2. Kisa cha "asshaabu quariya" katika Sura Yasin. 3. Nini yalikua malengo ya kisa cha "asshaabu quariya" kwa Mtume Muhamad? 4. Aya ya 13 maelezo na mifano yake. 5. Nini maana ya neno quariya? 6. Maswali na majibu. - Kufa na maelezo yake; -...
14 | Tafsir Surah Yaasin
1. Ni nani hawa Mitume aliyowapeleka Allah katika mji wa Antakiyyah? 2. Sababu zipi zilitolewa kwa Mitume waliopelekwa Antakiyyah ni Mitume ya Allah? 3. Sababu zipi zilitolewa kuwa hawa waliopelekwa mji wa Antwakia ni wanafunzi wa Nabii Issa? 4. Aya ya 14 ikieleza kisa "asshaabu quaruya" kwa tafsiri. 5. Yapi yalikua malengo ya kuletwa kisa...
15 | Tafsir Surah Yaasin
1. Vitu viwili vipi tusivisahau katika kusoma kisa hiki? 2. Mitume walijibu nini baada ya kupingwa na wapinzani wao kwa mujibu wa Sura Yasin? 3. Ni zipi tofauti kati ya Mitume na waja wa kawaida? 4. Njia zipi walizitumia wapinzani kuwapinga Mitume baada ya kudhihirisha Utume wao? 5. Majibu ya Mitume baada ya vitisho vya...
16 | Tafsir Surah Yaasin
1. Kauli na nasaha za mfuasi wa Mitume kwa wapinzani wa Mitume. 2. Sababu/dalili zipi alizotoa Allah kwa waja wa antwakia kuwakubali Mitume wake? 3. Sababu zipi ziliwafanya Mitume wasitake malipo kutoka kwa waja ulimwenguni? 4. Nini maana ujira alioungelea Mtume katika Sura Yasin? 5. Ni ujira upi Mtume aliuomba kwa waja katika Sura Yasin?...
17 | Tafsir Surah Yaasin
1. Maelezo ya ufupi aya 22-24 ya Sura Yasin. 2. Dalili zipi walizotoa wapinzani kupinga Mitume wa Allah? 3. Sampuli za watu wanaomuabudu Allah ni ngapi? 4. Maana na Fasili ya neno fatarani ni ipi? 5. Sababu zilizothibitisha Allah ndio anaestahiki kuabudiwa ni zipi? 6. Kazi za Mitume kwa umma ni zipi? 7. Nini hasa...
18 | Tafsir Surah Yaasin
1. Nani anahutubiwa na aya ya "inni amantu birabikum fasmahuun" katika Sura Yasin? 2. Nini walichokifanya wapinzani baada ya kuelezwa aya hii? 3. Maisha ya akhera ya mtu aliyenena aya ya "inni amantu birabikum fasmauun" kwa wapinzani wa Mitume. 4. Sampuli za ikram za Allah ni ngapi? 5. Faida zipi tuzipatazo kutoka kwa kisa cha...
19 | Tafsir Surah Yaasin
1. Nini kilichokua baada ya kuuawa yule mtu (habib najaar), kupingwa ile Mitume katika mji wa antwakia? 2. Habib najaar na kaumu zake. 3. Ni kipi kinachokanusha kushushwa katika mji wa antwakia? 4. Uangamizo/mwisho wa waja wa mji wa antwakia. 5. Hasara zipi wamezipata watu walioangamizwa wa antwakia? 6. Mafunzo gani tunapata kutoka kwa kisa...
20 | Tafsir Surah Yaasin
1. Maelezo ya mafungamano baina ya aya ya 32 na 33 za Sura Yasin. 2. Dalili zipi zaonyesha kuwepo kwa Allah? 3. Kwanini Allah ametumia "faminhum yakiruun" katika kuelezea chakula? 4. Kwanini Allah aliongelea tende na zabibu kuelezea matunda? 5. Maswali na majibu. - kwanini Allah aficha dalili za kuwepo kwake, kwanini asituthibitishie moja kwa...
21 | Tafsir Surah Yaasin
1. Maelezo ya aya ya 35 ya Sura Yasin. 2. Kwa nini Allah ametoa mahitaji yote ya waja ardhini? (nini malengo ya kuumbwa ardhi?) 3. Dalili ya shukran kwa yule anayetuneemesha na adabu zake. 4. Qur’an imetumiaje suala uhai na umauti kueleza mambo/kuthibitisha itikadi ulimwenguni? 5. Malengo ya kusoma uhai na umauti ya yapi? 6....
22 | Tafsir Surah Yaasin
1. Muhtasari mfupi wa darsa ilopita. 2. Ugumu wa somo la uhai kwa wanazuoni. 3. Pande mbili za miujiza ya viumbe hai ni zipi? 4. Miujiza ya mimea ni ipi? 5. Sampuli za mimea kama dalili ya kuwepo kwa Allah. 6. Fasili na maana za aya ya "subhanaradhina harakah azuwaja kullaha".
23 | Tafsir Surah Yaasin
1. Aya ya 37 na maelezo yake. 2. Rai nne kueleza dalili ya Allah na nguvu zake katika kupambanua usiku na mchna. 3. Ni yapi maumbile ya ulimwengu/ardhi? 4. Mjadala wa tafsiri kuhusu wau ya aya ya "washamsu...." katika Sura Yasin. 5. Rai 4 kuFasilii nyendo za jua zikusudiwao na Allah. 6. Sifa zipi alichagua...
24 | Tafsir Surah Yaasin
1. Mwezi kama dalili ya kuwepo kwa Allah. 2. Maumbile, steji na nyendo zipitiazo mwezi. 3. Nidham na kudra za Allah katika kuumba ulimwengu ni zipi? 4. Vipi Qur’an ilitumia vitu hivi vinne kuthibitisha kudra za Allah? 5. Faida za mchana, usiku, jua, mwezi ulimwenguni. 6. Maswali na majibu. - Hukumu ya nchi zinazokua na...
25| Tafsir Surah Yaasin
1. Ni vipi Allah anatenda kazi katika bahari? (nidham za bahari) 2. Kuna mfungamano gani kati ya aya hii (41) na aya zilizopita? 3. Fasili 3 tofauti za aya 41 na maelezo yake. 4. Nabii Nuh na kisa cha jahazi lake na umuhimu wake. 5. Umihimu(faida) za neema ya bahari ni zipi? 6. Vipi ilikuja/ilitengenezwaje...
26 | Tafsir Surah Yaasin
1. Muendelezo wa maelezo ya neema ya bahari. (usafiri baharini) 2. Ni vipi bahari yachangia chakula cha viumbe ulimwenguni? (tani ngap?) 3. Ni vipi bahari yachangia hali ya hewa ya ulimwengu? 4. Ni upi mchango wa bahari katika kuleta afya ya waja ulimwenguni? 5. Maajabu yaliyoumbiwa bahari ni yapi? 6. Fasili na maelezo ya aya...
27 | Tafsir Surah Yaasin
1. Fasili na maelezo ya mwanzo ya aya ya 45. 2. Nini maana ya kuucha vilivyombele yetu na nyuma yetu? 3. Rai 6 zinazoeleza nini cha kuuchwa mbele na nyuma ya waja ulimwenguni. 4. Makosa gani adhabu zake zatolewa hapahapa ulimwenguni? 5. Sera na nyendo za wapinzani dhidi ya kupinga Mitume. 6. Irada ngapi za...
28 | Tafsir Surah Yaasin
1. Ni maudhui gani yamechukuliwa na juzuu hii ya Sura Yasin? 2. Fasili na maelezo ya aya ya 48 ya Sura Yasin. (maneno ya wapinzani wa Mitume) 3. Ni lini hiko kiama? je kipo au hakipo? 4. Kwanini imani ya siku ya kiama na maisha ya akhera ni msingi mkubwa wa imani ya uislam? 5....
29 | Tafsir Surah Yaasin
1. Sababu kwa nini Allah alificha lini kiama kitakuja. 2. Ni vipi Allah/Qur’an iliwajibu wapinzani kuhusu upinzani wao wa kufufuliwa waja siku ya kiama. 3. Vipi Allah aihusisha ardhi baada ya mauti? 4. Ni ipi mifano ya kiyama ipitayo mbele ya waja ulimwenguni? 5. Je kufufuliwa ni kwa roho na mwili au roho tu?
30 | Tafsir Surah Yaasin
1. Maelezo ya steji za siku ya kiama. 2. Ni nidham gani itafuatwa katika kuhesabu mizani ya waja siku ya kiama? 3. Kwanini mahakma ya siku ya kiama itaendeshwa kiuadilifu? 4. Nukta 3 muhimu za aya ya 54 ya Sura Yasin ni zipi? 5. Nini maana ya uadilifu? ni upi uadilifu wa Allah kwa waja?...
31 | Tafsir Surah Yaasin
1. Manzira ya mwisho baada ya mahesabu siku ya kiama ni yapi? 2. Kwanini msingi wa starehe za pepo ni lazima ue na utulivu wa kinafsi? 3. Maelezo ya starehe za kimwili za peponi. (mke/mume ,hulullain,chakula) 4. Maelezo ya starehe za kinafsi za peponi. 5. Kwanini masihara ya kuamini pepo na moto ni itikadi muhimu...
32 | Tafsir Surah Yaasin
1. Muendelezo wa malipo ya amali njema za wasio waislam. 2. Madhumuni na fikra zilizotukuziwa aya za kueleza pepo ni zipi? 3. Sampuli mbili za ukaffir na maelezo yake. 4. Ni zipi steji za kujisalimisha kwa mja kwa Allah? 5. Sifa mbili zipi zatumiwa kutengamaa jambo kama ni zuri au si zuri? 6. Sampuli za...
33 | Tafsir Surah Yaasin
1. Muendelezo wa sampuli za starehe za peponi na maelezo yake. 2. Mijadala je pepo na moto vishaumbwa au bado? 3. Je kama pepo/moto zimeumbwa zitatoweka au la? (baada ya gharika za kiama) 4. Masihala ya rataba/kuchoshwa kwa binadam na starehe za pepo. 5. Kwanini mtu hawezi kukidhi kima cha kitu mpaka akikose? 6. Aya...
34 | Tafsir Surah Yaasin
1. Ni nani hao watu wa motoni? 2. Ni zipi sababu zitawapelekea watu kuingia motoni? 3. Nini hakika ya moto? 4. Nini maana ya sakar? 5. Majina ya moto. 6. Je kuna sababu/haja gani za kuwepo na huu moto?
35 | Tafsir Surah Yaasin
1. Kuna milango mingapi ya moto? 2. Ni nini maksudio ya kua na milango ya moto? 3. Ni zipi sampuli za adhabu za watu wa motoni? 4. Ni nani watakaoketi milele motoni? 5. Ni vipi madhambi huvutia madhambi mengine? 6. Ni vipi ushahidi wa matendo utaonyeshwa mbele ya waja siku ya hesabu? 7. Sampuli za...
36 | Tafsir Surah Yaasin
1. Fasili na maelezo ya aya za kwanza za juzuu ya tano. 2. Adhabu 2 gani ambazo Allah aliwatisha watu wa Makka kwa matendo yao? 3. Kwanini twapaswa kushukuru kwa kila neema kutoka kwa Allah? 4. Ni neema zipi ambazo waja hatudhithamini mpaka tuzikose? 5. Kwanini Mtume Muhammad (S.A.W) aliwapa majukumu makubwa vijana(barobaro) na si...