KUHUSU ILM

Karibu katika Ilmafrica, ni tovuti inayo elimisha jamii kuhusu maada na mijadalo mbali mbali kutoka Quran, hadithi za Mtume na historia ya kiislamu.

Tunawakaribisha kuanza safari ya kubofya ili kuchunguza (mambo) yaliyomo kwa ukamilifu, tunatumaini kwamba safari hii ni chanzo cha elimu na ujuzi na kama bohari ya hazina ya kuendeleza elimu yako zaidi kuhusu Uislamu

Madhumuni makubwa ni kusaidia uenezaji wa elimu kupitia njia hii ya mtandao kwenda kwenye maeneo ambako vyanzo kama hivi kwa kawaida huwa havipatikani kwa urahisi. Kwa nyongeza tunalenga kushawishi utafiti na kulizia taarifa ambazo husaidia katika matumizi ya tekinolojia.

Kwa kuanza safari yetu kwa sasa tumepakua tu video za Sheikh Aidarusi wakati ambapo juhudi za lazima zinafanywa kuongeza wazungumzaji wengine.

Kigezo: Kwa mtandao huu wa Ilm Africa, tunajaribu kuwasilisha picha mizania na sahihi ya Uislamu kama ambavyo umetekelezwa na kufundishwa na Mtukufu Mtume Muhammad (saww) na familia yake na sunna. Juhudi zote za maana zimefanywa ili kuzuia taarifa zisizo sahihi kuchukuliwa katika tovuti hii.