SEHEMU 24
Tukiwa twaendelea na mada yetu na tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
Bado twazungumzia niyapi ya kufikiriwa Jana tulizungumza kitu cha kwanza kinacho takiwa kufikiriwa kwa mwanaadam muislam tukasema ni qurani.
( 1 ) Leo tumalizie katika kuangalia qurani ambayo ni kitu cha kwanza kufikiriwa. Katika surati SWADI aya 29 m/mungu asema ( hii qurani nikitabu, m/mungu amekiteremsha kwako ambacho nikitabu kimebarikiwa wapate kuzingatia aya zake na wapate kuwaidhika wale wenye akili)
( 2 ) Kwahiyo katika aya hiyo m/mungu awataka watu waislam waelekeze akili zao, kwenye qurani,na wale wenye mazingatio basi wazingatie hii quran.
( 3 ) Suratu Muhammad Aya ya 24 m/ mungu asema ( na hawazingatii hii qurani ama hawa nikatika wale ambao nyoyo zao zimefungwa.) Hivyo ngugu zangu aya ninyingi sana zinazo wataka waislam kufikiria juu ya kitabu hiki. Nasisi tumefupisha tu nilimradi kuwafahamisha watu yanayo paswa kufikiriwa.