SEHEMU 23
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
Tuangalie swali letu la pili lisamalo niyapi ya kufikiriwa?
( 1 ) Yakufikiriwa ndugu zangu nimengi sana hayana idadi ila ili tuweze kuelewana vizuri tuyagawe mambo katika sehem tatu yakufikiriwa.
( 2 ) Sehem ya kwwnza ni KITAABUL_MAQRUU. nikitabu chenye kusomwa,kama tulivyo eleza mwanzo. Pili ni NIKITABUL_KAUN. Kitabu cha ulimwengu. Tatu ni KITABUL_ INSAAN. kitabu cha mwanaadam.
( 3 ) Tukianza na kitabu chenye kusomwa yani quran. Kitu chakwanza kwa mwanaadam muislam anachotakiwa kufikiria,kukizingatia nihiki kutabu cha quran. Kama asemavyo m/ Mungu katika suratil_ Annisaai aya 82 (hawa izingatii hii quran,ingekua yatoka kwa asie kua m/Mungu wangelikuta kasoro nyingi.)
( 4 ) Katika aya hiyo m/Mungu anatuonesha kua qurani nikitabu kinacho takiwa kufikiriwa maana yake, makusudio yake, aya zake. Naili muislam moyo wake uwe safi lazima atie ndani yake qurani. Nayapaswa kila mmoja kuijua qurani,na kuusoma.