SEHEMU 22
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
( 1 ) leo tuangalie je khabari zinazo letwa na akili au maarifa anayo yapata mwanaadam kupitia chombo cha akili yaweza kutegemeka kielim?
( 2 ) wako wanao pinga kua chombo hiki si chakutegemeka katika kupata maarifa.
( 3 ) Wasema hatuwezi kutegemea akili katika kupokea maarifa. Kwasababu wenye akili wenyewe hutofautiana katika hayo mambo ya kiakili. Kama wana falsafa mfano.
( 4 ) Lakini katika majibu ya yakulijibu hili nikua ikiwa kutofautiana kwa wanachuoni nisababu yakuto kusihi kwajambo nakutegemewa. Basi haifai kutegemea elim hata moja. Kwani hakuna elim yeyote ambayo wataalam wa elim hiyo hawaja tofautiana.
( 5 ) Pili kutofautiana kwa wanachuoni,wanafikra kutokana na jambo sio lamaanisha kua jambo lile si sahihi bali lamaanisha kua baadhi yao hao hawaja tumia misingi sahihi yakufaham hilo jambo.
( 6 ) Hivyo ndugu zangu akili inathamini kubwa nandio qurani ikatutaka tuitumie pale m/mungu asemapo ( Afalaa taaqiluun) au ( Lau kunna nasmau au naaqilu.)