SEHEMU 21
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
Baada ya kufaham vyombo vinavyo isaidia akili kufikiri leo ndugu zangu kabla ya kuingia katika kufaham niyapi ya kufikuriwa tuangalie kwanza je hivi vitu vinavyo saidia akili kufikiri vinauwezo wa kumpatia mwanaadam elim?
( 1 ) Dekarti mwanafalsafa huyu yeye asema hisia hizi tano haziwezi kumpatia mwanaadam elim nasio vyombo vya kutegemewa. Kwanini? Asema nikwasababu hisia hizi tano kuna wakati zakosea,yani zinakupa ufahamu wa kimakosa.
( 2 ) Lakini tumeona qurani nijinsi gani imetaja kua nivitu muhim na ndio vyombo vinavyo mpatia mwanaadam elim na maarifa,ikiwemo aya katika suratil Annahli aya 28.
( 3 )Wanachuoni wasema pale mwanaadam anapokua anakosoa hisia tano.kua zakosea basi afaham kua kuna yahakika yameonekana na jicho au yameskika na skio au na hisia zingine. Yale ya hakika ndio yamempa elim yakua haya nimakosa. Lakini yote hayo yameletwa na hisia tano. Hivyo hisia tano zategemewa katika kumpatia mwanaadam elim.