20 | KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU

SEHEMU 20

Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.

Bodo twazungumzia sehem ya swali letu la kwanza lisemalo vipi tutafikiri.?

( 1 ) Jana tulizungumzia Aya ya suratul Annahli aya 28. Katika aya hii m/mungu ataka kutuonesha mambo mawili kwanza atufahamisha kua ametutoa katika matumbo ya mama zetu ilihali tukiwa hakuna tulijualo. Pili atufahamisha kua ametupa maskio,macho,na akili kwaajili yakupokelea elim na kufahamia vitu.

( 2 ) Utaona katika aya hiyo m/mungu amezungumza skio kwa (mufradi) umoja halafu macho akayazungumza kwa wingi. Niipi hekma yake?

( 3 ) Moja ya hekma japo m/mungu afaham zaidi nikua yani mwanaadam chombo kinacho mletea elim zaidi nimacho yake. Ndio m/mungu akakileta chombo hicho kwa njia ya (jamuu) wingi.

( 4 ) Hivyo ndugu zangu mpaka hapa tumefaham mwanaadam ili aweze kufikiri chombo chakwanza kabisa kinacho kuja kumsaidia katika fikra zake ni chombo kiitwacho hisia kwamaana yake ya kawaida na kwamaana ya kielim.