SEHEMU 19
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
Leo tuangalie vipi tutafikiri na niyapi yakufikiriwa.
( 1 ) Tuanze na kujiuliza vipi tutafikiri? Baada ya kua tumefaham maana ya kufikiri,na umuhimu wa fikra,na ulazima wa kufikiri sasa nivipi tutafikiri?
( 2 ) Ndugu zangu ili tuweze kujua nivipi tutafikiri, kwanza kabisa yatupasa tufahamu vyombo vinavyo isaidia akili katika kufikiri.
( 3 ) M/mungu asema katika suratil_Annahli aya 28 ( m/mungu amewatoeni nyinyi katika matumbo ya mama zenu ikiwa hamjui chochote, kisha akawapa maskio,na macho, na kifua.(akili) ili nyinyi mshukuru.)
( 4 ) Hivyo m/Mungu katika aya hiyo anatuonesha vyombo vya kufikiri. Usije ukachukua laskio ukapeleka kwenye macho na lamcho ukapeleka kwenye skio,au yaskio namacho ukayapeleka kwenye akili, bila shaka fikra zako zitakua zamakosa.
( 5 ) mtu hawezi kufikiri mpaka awe na mambo anayo yajua katika akili yake ili yamsaidie kuyajua yale ambayo anataka kuyafahamu. Kama tulivyo sema nyuma.