SEHEMU 17
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU. Bado tupo na swali letu nini umuhimu wa kufikiri?
( 1 ) Tulisema ili tuweze kujibu swali hili yapaswa tufaham vitu vitatu ambavyo ni MWILI,ROHO,AKILI.
( 2 ) tukaeleza mwili na mahitaji yake japo kwa uchache,pia tukaeleza roho na mahitaji yake japo kwa uchache. Ambacho kitu chakwanza kabisa katika mahitaji ya Roho ni (amani kutokana na khofu.)
( 3 ) Leo tuanagalie kitu cha mwisho katika vitu hivi vitatu, nacho ni Akili. Akili nayo inamahitaji yake, kama ambavyo m/mungu ametutaka tuushibishe mwili na roho. vile vile ametutaka sisi tuishibishe akili yetu.
( 4 ) M/mungu ametutaka tuishibishe akili yetu kwa elimu pale alipo sema katika suratil Al-alaq aya 1 (soma) pia tuishibishe kwa ubunifu na uvumbuzi, na tuishibishe kwa fikra. (Afalaa yandhuruna ilal_ibili kayfa khuliqat.) Je hwafikilii kuhusu ngamia namna gani ameumbwa.
( 5 ) Mwisho twahitaji fikra na nimuhim sisi kufikiri. kwakua fikra nikatika chakula cha Akili. Akili ambayo ndio kiongo cha tatu kinacho kuja kumkamilisha mwanadamu.