SEHEMU 16
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU. Bado twazungumzia umuhim wa kufikiri
( 1) Nukta ya pili katika upande huu wa umuhim wa kufikiri nikujiuliza niipi haja ya sisi wanaadam kufikiri.?
( 2 ) Katika vitu vikuu vilivyo mkamilisha mwanaadam ni mwili, roho,na Akili. Tukiweza kufaham kila kimoja katika vitu hivi vitatu,na tukakipa kila kimoja haki yake basi tutafaham umuhim wa Mwanaadam kufikiri.
( 3 ) Tukianza na mwili… MWILI twamaanisha nikiwili wili ambacho kimetengenezwa (kimada) kinacho onekana na ambacho kimejengwa juu ya tabia kama kula na kunywa, pia kama kupenda kuishi milele,pia kama kupenda kumiliki nk.
( 4 ) Ama Roho ya mwanaadam twapata mahitaji yake katika suratil QURAYSHI Aya ya mwisho kua ni Amani (utulivu) umuhim wa sisi kufikiri waja vipi sasa?