15 | KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU

SEHEMU 15

Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU. Baada ya kuangalia maana ya fikra.

Leo tuangalie umuhimu na ulazima wa kufikiri kwa mwanaadam.

( 1 ) Kufikiri kwa mwanaadam ninishati kwake ya uchangamfu,ambayo yategemea aina ya tatizo linalo mkabili hilo moja.

( 2 ) Pili watuambia wanachuoni kua watu wote hufikiri kwani mwanaadam hautimu ubinaadam wake bila ya kua nachombo hiki kiitwacho fikra.laikini niwachache wanao fikiri fikra sahihi. Kwani kufikiri nisilaha yainayowapatia watu mazingatio yakuwamufaisha. kufikiri nichombo kinacho weza kuzalisha maadili ya kufaidisha jamii ya wanaadam.

( 3 ) Na umma ili uweze kupiga hatua lazima uwe na vitu viwili kwanza uwe na fikra yenye matunda kwa umma. pili nikua na mazingatio kwayale yaliyo pita nyuma.

( 4 ) Mwisho ndugu zangu twapata umuhim wa kufikiri pale m/mungu alipo sema kua amewapatia wanaadam kitu ambacho viumbe wengine hawakupewa (fikra) suratul_israa ya 70.