SEHEMU 14
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
( 1 ) Bado twaendelea katika kujibu swali lisemalo kufikiri ninini?
( 2 ) Jana tulieleza maana ya kilugha (kiarabu) leo tuangalie maana ya kisheriya (kielim) ampako tutaangalie watu wa SAIKOLOJIA na watu wa TARBIYA(malezi) na watu wa MANTIQ.
( 3 ) Watu wa saikoji wasema-kufikiri ni nikuzitumia nyadhifa za kinafsi za kufikiri wakati unapo taka kutoa suluhu ya tatizo miongoni mwa matatizo husika.
( 4 ) Watu wa tarbiya(malezi) husema -kufikiri nikila harakati ya kiakili yenye lengo maalum katika kutatua matatizo au katika upande wa kutafsiri tukio flan.
( 5 ) Watu wa elim ya mantiq. Wao husema – kufikiri ni wakati akili yako inapo tembea kutokana na mambo unayo yajua, kwenda kwenye yale usio yajua.
( 6 ) Hivyo ndugu zangu kufikiri nikutumia akili yako kuchukua yale unayo yajua ili yakusaidie kuyafaham yale ambayo huyajui. Na hili latofautiana kutokana na akili za watu yule ambae akili yake itakua kubwa basi na kufikiri kwake kutakua juu. Tofauti na mwenye akili yachini.