13 | KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU

SEHEMU 13

Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.

( 1 ) Tukiwa bado twazungumzia maana ya fikra ni nini? Leo tuangalie neno fikra kwa upande wa kilugha (kiarabu)

( 2 ) Fikra kwa upande wa lugha(kiarabu) wataalam wa lugha ya kiarabu watuambia kua yamaaniaha (Attaammul) kupeleleza jambo. Au kuifanyisha kazi akili, Au nikuchukua yale unayo yafaham ili kukusaidia kujua yale uasio yafaham ili upate nayo kuyafaham.

( 3 ) Ama kwa upande wa kisheriya ( kielim) neno hili limetizimwa na wanavyuoni wengi sana, nakila mtu akalieleza kwa mtazamo wake

( 4 ) Kwasababu kuna watu hufikiri kwa kiwango cha chini huyu anafaham fikra kwa maana yake. Na yupo anae fikiri kwa kutumia akili peke yake, nayupo anaefikiria kwa kutumia moyo na akili na Ilham, kutoka kwa Allah/wote waha hawezi kua sawa katika kuelewa maana ya kufikiria. Ninacho jaribu kusema nikua neno fikra kwaupande wa kielim/kisheriya lina taarifu tofauti tofauti.