SEHEMU 12
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
Baada ya kuangalia maneno yaliyo tumika ndani ya qurani yakiwa yanamaana sawa na kufikiri sasa twaingia katika maana ya fikra fikra nini?.
( 1 ) Lakini kabla hatujaingia katika jibu la fikra nini kwanza tuangalie chombo kinacho tumika katika kazi ya kufikiri nini?
( 2 ) Maulamaa hutuambia chombo kinacho tumika katika kufikiri ni Akili japo kuna vinginevyo ila kikubwa ni akili.
( 3) Ni nini hii Akili? Asema Shekh muhammad Rayshahary katika kitabu chake mabaanul- maarifa kua akili ni (markazil-fikra) nichombo cha fikra. Akili nikatika vitu alivyo viunba m/mungu kwa maumbile ya kimada (haionekani)
( 4 ) Akili kwa maana ya kilugha ( kiarabu) yamaanisha (Alhabsi) kufunga. Wasema imeitwa akili kwa maana hii.kwakua yamzuia mwanaadam kufanya yasio kua sawa nayeye. ( 5 ) Akili katika upande wa kisheriya( kiislam) yamaanisha (ghariza) tabia inayo msukuma mtu kufanya jambo fulani. Hii ndio akili.