11 | KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU

SEHEMU 11

Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.

Leo katika kukamilisha mazungumzo yetu yajana mbayo tulikua twazungumzia AL-QALBU. (Moyo)

( 1) Tumalizie kwa kuangalia hadithi ya Imaam Jaafar swadiq {a.s} yeye atuonesha Mafungamano makubwa yaliyoko baina ya akili/fikra, moyo, nahisia.

( 2 ) Asema ( Imani ya mtu haiwezi kutimia mpaka moyo wake unyoke, nahauwezi moyo wake kunyooka mpaka ulimi wake unyooke.)

( 3 ) Imam alipo sema neno imani hapa akusudia Akili/ fikra. Yani akili ya mwanaadam haiwezi kuwa sawa bila ya moyo,nawala moyo wake hauwezi kuwa sawa bila ya kua sawa ulimi wake yani (hisia)

( 4 )Hivyo kwa hadithi hii ya imam swadiq twafaham Neno moyo katika quran. mara limekuja likiwa na maana ya kituo cha hisia,na mara likiwa na maana ya akili/fikra,na mara likiwa na maana ya ushirikiano kati ya moyo hisia na akili.