SEHEMU 10
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
Leo tuangalie neono ALQALBU natuishie hapa katika kuangalia maneno yaliyo namaana ya kufikiri/kutumia akili ndani ya qurani.
( 1) Neno qalbu limetumika katika qurani mara 132 nawengine maulamaa husema nizaidi ya hiyo bali ni mara 144.
( 2) Lakini pamoja na yaote hayo ila tuelewe kua Neno hili lime tajwa mara nyingi sana katika qurani tukufu.
( 3 ) Miongoni mwa maeneo ambyo limekuja neno hili likiwa na maana ya kufikiri/kutumia akili ni katika suratil Alhajji aya 46.nakatika suratil aarafu aya 179. Nakatika suratil qaafu aya 37
( 4 )Ibnu mandhuur asema moyo wakati mwingine wamaanisha akili katika lugha ya kiarabu. mfano wa suratul qaafu aya 37. M/mubgu asema (nakatika hilo kuna ukumbusho kwa yule mwenye moyo. Ukiangalia kila mwanaadam anamoyo sasa m/mungu amaanisha moyo ule wenye kutumika.
Yaani yule mwenye kutumia akili.