SEHEMU 9
Leo bado, twaangalia maneno yaliyo tumika katika qurani ikimaanisha akili/fikra. Nalo ni AL_HEKMA.
( 1) Wanachuoni watuambia neno hili limetumika katika qurani mara(20) pia neno (HAKIIM) ambalo nisifa ya Hekm neno hili limetumika mara (98) lakini si kila itumikapo.hekma yamaanisha akili/fikra, Hapana. Bali utakuta sehem ambayo yahusu akili/fikra.nipale linapo kuja neno hekma huku limetanguliwa na neno (kitaabu) au (aayaat) mafano suratil baqara aya {196}
( 2 ) Hekma kwa maana ya kilugha (kiarabu) linamaanisha uadilifu/upole/ na kizuwizi/kuweka kitu mahala pake. Hiyo ni maana ya lugha(kiarabu)
( 3 ) Kisheriya katika uislam neno hekma lafaamika kwa maana ya ( qudrat aqliyat) uwezo wa kiakili wakuweza kufanya jambo sawasawa nalinavyo takiwa kufanywa. Hivyo moja ya maana ya hekma katika qurani yamaanisha akili kwakua miongoni mwa maana ya hekma ni kuzuia Na akili humzia mtu kufanya mambo mabaya pia vile vile hekma yamzuia mtu kufanya mambo mabaya.