SEHEMU 8
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
Leo bado, twaangalia maneno yaliyo tumika katika quran yakimaanisha kufikiria, Kutumia akili. ANNADHWAR, na BASWIIRA.
( 1 ) Neno Annadhwar, Maulamaa watuambia pamoja na maana tofauti tofauti limetajwa mara {104,}ndani ya quran.
( 2) Annadhwar, limetumika kwa maana nyingi takribani maana( 6 ) lakini katika surutil Al_anaam aya [11] Hapa utakuta aya hiyo yatutaka sisi tutumie akili tufikirie katika mabo yaliyo pita nayaliyoko sasa. Hilo ni neno Annadhwar, ambalo limekuja mara moja tu likiwa na maana ya kutumia akili,kufikiria. Japo limekuja mara nyingi nakwamaana nyingine.
( 3 ) Ama neno BASWIIRA. hili limekuja ndani ya qurani pamoja na maana tofauti tofauti, mara 148 miongoni mwayo ni aya inayo patikana katika suratil hashri.
( 4)katika suratil Hashri aya (2) M/mungu asema ( faatabiruu yaa ulil_Abeswaar.) Zingatieni enyi watu wenye kutumia akili. Imekua abeswaar, kwa maana ya kufikiri kwakua imetanguliwa na. Mazingatio.