07 | KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU

SEHEMU 7

Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.

Leo bado, twaangalia maneno yaliyo tumika ndani ya qurani yamanisha watu watumie akili zao, fikra zao.

( 1 ) Pia kuna neno ANNUHA Neno hili katika qurani limetumika mara 2 tu. Aya hizi zapatikana katika suratil Twaha aya 54 na aya 128.

( 2) Swali la kujiuliza ANNUHA Lina maana gani? Ibnu farsi mtaalam wa lugha ya kiarabu asema :annuha inamaanisha (kizuizi) akaendelea kusema nakwaajili hiyo inaitwa akili. Annuhya kwakua akili yamzuia mtu kufanya maovu. ( inna fii dhaalika laa yaati liuli nnuha)

( 3 ) Lingine ni neno ALHIJRI neno hili limetajwa mara moja ndani ya quran, katika surat fajri (halfii dhaalika qasamul llidhii hijri.)

( 4 ) Lingine ni AL_AHLAAM hili limekuja mara moja tu ndani ya qurani suratul Tuur aya 32. lamaanisha akili, ama kwa maana nyingine limekuja mara nyingi tu.

( 5 ) Neno la mwisho kwaleo ni Atadaburi neno hili limetajwa katika aya 4.ndani ya qurani suratul Annisaai aya 82.suratul muuminuun aya 68. Suratul swad aya 29. Suratul muhammad aya 24.