SEHEMU 5
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
Leo tuangalie ile njia ya tano katika mazungumzo yetu ya jana. Ambayo ilikua ikisema, Kwa kuwalaum wale ambao hawatumii akili zao, fikra zao.
1. Katika suratil aarafu aya(179) rejea vizuri sana aya hiyo utakuta m/Mungu azungumzia vipi wanadamu wataingia katika.moto wa jahannam. Nikwasababu yakuto kutumia akili .
2. Ikiwa sababu ya kuto kutumia fikra,akili. nisababu ya kuingia motoni. Hapa twapata faida zifuatazo.
3. Moja kuto kufikiri,nakutumia akili yako nikatika madhambi makubwa.
4. Pili twapata kuelewa kua kufikiria, kutumia akili nikatika wajibu ulio.wajuu zaidi katika uislam mpaka kupelekea kuwachwa kwake yapelekea kupata adhabu za Allah.
5. MWISHO m/Mungu. Katika suratil jaathiya, aya (13) asema ( M/mungu ameweka chini ya utumishi wenu (milki) yale yaliyoko mbinguni na ardhini vyote. Hakika katika hayo kuna dalili kwa watu.wenye kufikiri.)
6. Ili upate faida ya uwepo wa mbingu na ardhi na vilivyomo lazima utumie akili,fikra