04 | KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU

SEHEMU 4

Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU. leo tuangalie ni usulubu upi (njia) zipi zilizo tumika katika qurani,zikitutaka sisi tutumie.akili,tufikirie

1. Pindi qurani inapo tutaka sisi tutumie akili, fikra, kuna njia tofauti tofauti imetuma yakwanza ni AMRI(maamrisho.) Kama katika surat (Abasa) m/mungu asema (naangalie mwanaadam kwenye chakula chake….) Utaona hapa kuna irada ya Mungu akikutaka wewe utumie akili yako fikra zako kuchunguza kunanini katika chakula?.

2. Njia ya pili ni ISTIFHAM (kuuliza) Lakini m/Mungu si kama auliza anataka majibu yake, hapana bali nimaulizo ya kukupa tanbiihi (ukumbusho) nawakati mwingine kukutisha. Kwanini hauitumii akili yako ,fikra yako?kama AFALAA YAAQILUUN(Je hamtumii akili?

3. Njia ya tatu ni njia ya VIAPO m/Mungu akitutaka tuangalie ndani ya vitu hivyo anavyo APA kwavyo vina faida gani.

4. Najia ya nne qurani imetumia njia ya kutupa mifano ya picha mbali mbali kama wanyama nk.

5. Najia ya tano namwisho nikulaum wale walioshindwa kutumia akili,fikra zao.