SEHEMU 3
Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.
Leo tuangalie akili nafasi yake ilivyo tumika katika quran. Na fikra nafasi yake ilivyo tumika katika quran.
1. Tukianza na akili. Akili imezungumzwa katika qurani sio kwa kutajwa (ismu) kwajina lake. Bali limetajwa kwa (swiigha) kwa kazi ya akili.
2. Yani maana ya kutajwa kwa sampuli hii katika qurani wanachuoni watuambia m/Mungu ataka kutujulisha kua umuhimu sio tu kua na akili bali ni matumizi ya hiyo akili. Na neno akili limetajwa ndani ya qurani mara 49.
3. Ama fikra limetajwa ndani ya qurani mara 18 Kuna baadhi limetumika kama (FAKKARA) mara 1 tu ndani ya quran, katika Surat Almuddathir.
4. mara limetajwa kama (TATAFAKKARUU) mara 1 katika suratil_sabai. ikiwa na maana ya kufikiria mara kwamara. Mara limetajwa kama TATAFAKKARUUNA mara 3 na YATAFAKKARUUNA mara 2 Na YATAFAKARUU mara 11. Kwahiyo utaona ni jinsi gani qurani imeipa kipaombele sana akili ya mwanaadam ama fikra ya mwanaadam. Katika dauru, mzunguko wa maisha yake.