02 | KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU

SEHEMU 02

Tukiwa twaendelea na mada yetu tulieipa jina ya KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU.

leo tuangalie QURANI imelitizama vipi swala hili la kufikiri kwa mwanaadam.

1. Yani je huku kufikiri kutumia akili, kumepewa kipao mbele katika QURANI? M/mubgu asema katika surat sabai aya ya 76 (kaeni wawili wawili au mmoja mmoja kisha mfikiri)

2. Qurani nikitbu pikee kilicho shugulika mno na swala la kutumia akili kufikiri,mpaka kufikia kuwaita watu wasio tumia akili wasio fikiria, kua hao nikama WANYAMA, tena hata wanyama ni bora kwao.

3.Tufaham kua hakuna sheria ya kiislam itatekelezwa kama hakuna akili yani sheria ya kiislam imesimama juu ya kuwepo akili au kutoa kuwepo. Kwasababu kulipwa thawabu au kuadhibiwa kumesimama kwa misingi ya kuwepo akili au kutokuwepo akili.

4. Kama asemavyo bwana mtume Muhammad (s.w.w.w) ( hakika kheri yeyote hudirikiwa na akili, nahakuna dini kwamtu ambae hana akili

5. Mwisho qurani yaitaja akili katika upande wa kuitukuza, au kuikubusha au kuilaumu. Kama ambavyo tutakuja kuona mbele katika mfululizo wa darasa zetu hizi, inshaallah.