SEHEMU 1
leo nimependa tuzungumzie mada itwayo KUFIKIRIA KATIKA QURANI TUKUFU. Lakini kabla ya kuingia katika mada hii, kwanza tufaham hii qurani nikitabu gani?
1. Allah ameweka katika dunia hii vitabu viwili. Moja 1-ni kitabul kaun.(ulimwengu) yani jua mwezi nyota mbingu Ardhi navibginevyo. vinatengeneza kitabu hiki (Alkaun)
2. mbili QURAN (kitabu cha ALLAH kitukufu alikishusha kupitia mtume wetu muhammad, s a.w.w) Kitabu hiki twaweza kukishika kuhesabu herufi zake,karatasi zake, lakini maana yake na siri zake za ndani hatuwezi kuzihesabu. Wana chuoni leo hii pamoja na wingi wa vitabu vyao ila bado hawajafikia hakika yake kwanini?
3. Ni kwasababu nikitabu kimekuja kumjenga mwanaadam kua kiongozi duniani na akhera. Bwana mtume s.w.w. asema katika quran kuna maana ya dhwaahir (nje) na kuna maana ya baatwin(ndani) Maana ya nje, yani unapata hukmu za m/Mungu Na maana yake ya ndani, unapata elim. Hii ndio qurani ambayo twataka sisi twende nayo katika mada yetu ya kufikiria katika quran.