Sura hii imeteremshwa Madina, na ina Aya 8
Kwajina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake.
2. Na ikatoa ardhi mizigo yake.
3. Na mtu akasema: Ina nini!
4. Siku hiyo itatoa khabari zake.
5. Kwa kuwa Mola wako ameiamrisha.
6. Siku hiyo wataondoka watu wametawanyika ili waonyeshwe vitendo vyao.
7. Basi anayefanya wema sawa na chembe atauona.
8. Na anayefanya uovu sawa na chembe atauona.