Surah Yusuf

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 111

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

1. Alif Lam Ra. Hizo ni Aya za Kitabu kinachobainisha,

2. Hakika sisi tumeiteremsha Qur’an kwa uwazi ili mpate kufahamu.

3. Sisi tunakusimulia simulizi nzuri sana kwa kukufunulia Qur’an hii na ijapokuwa ulikuwa kabla ya haya miongoni mwa wasio na kahabari.

4. Yusuf alipomwambia baba yake: Ewe baba yangu hakika mimi nimeona (katika ndoto) nyota kumi na moja na jua na mwezi, nimeviona vikinisujudia.

5. Akasema; Ewe mwanangu! usisimulie ndoto yako kwa nduguzo, wasije wakakufanyia vitimbi. Hakika shetani kwa mwanadamu ni adui dhahiri.

6. Na hivyo Mola wako atakuchagua na kukufundisha hakika ya mambo na kutimiza neema yake juu yako na juu ya kizazi cha Yaakub, kama alivyoitimiza zamani juu ya baba zako Ibrahimu na Is’haqa. Hakika Mola wako ni Mjuzi, Mwenye hekima.

7. Kwa hakika katika Yusuf na ndugu zake yako mazingatio mengi kwa wanaouliza.

8. Waliposema: Hakika Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi hali sisi ni kundi lenye nguvu. Hakika baba yetu yumo katika upotovu dhahiri.

9. MuueniYusuf na mtupeni nchi (ya mbali) ili uso wa baba yenu ukuelekeeni, na baada ya haya mtakuwa watu wema.

10. Akasema msemaji kati yao: Msimuue Yusuf, lakini mtupeni katika shimo la kisima kirefu watamuokota baadhi ya wasafiri, ikiwa nyinyi ni wenye kufanya.

11. Wakasema: Ewe baba yetu! mbona hutuamini juu ya Yusuf na hakika sisi ni wenye kumtakia wema.

12. Mpeleke kesho pamoja nasi, ale kwa furaha na acheze, na bila shaka sisi tutamlinda.

13. (Baba yao) akasema: Kwa hakika linanihuzunisha nyinyi kwenda naye na ninaogopa (asije) mbwa mwitu akamla hali nyinyi mumeghafilika naye.

14. Wakasema: Ikiwa mbwa mwitu atamla na hali sisi ni kundi lenye nguvu basi bila shaka tutakuwa wenye khasara.

15. Basi walipomchukua na wakakubaliana kumtia katika shimo la kisima kirefu, na tukampa Wahyi (Yusuf) bila shaka utawaambia jambo lao hili hali hawatambui.

16. Na wakaja kwa baba yao usiku wakilia!

17. Wakasema: Ewe baba yetu! hakika tulikwenda kushindana mbio na tukamwacha Yusuf penye vyombo vyetu, basi mbwa mwitu akamla, lakini huwezi kutuamini ingawa tunasema kweli.

18. Na wakaja na kanzu yake ina damu ya uongo. (Baba yao) akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini kutenda jambo, basi subira ni njema, na Mwenyeezi Mungu ndiye aombwaye msaada juu ya haya mnayoyasema:

19. Na ukafika msafara wakamtuma mteka maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake, akasema: Ee furaha njema! Huyu hapa mvulana! nao wakamficha (ili kumfanya ni) bidhaa, na Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi wa wanayoyatenda.

20, Na (Ndugu za Yusuf) wakamuuza kwa thamani hafifu kwa pesa kidogo na hawakuwa na haja naye.

21. Na yule aliyemnunua katika Misri akamwambia mkewe: Mtengenezee makazi ya heshima, huenda akatufaa au tutampanga kuwa mtoto. Na hivyo ndivyo tulivyomkalishaYusuf katika nchi, ili kumfundisha hakika ya mambo, na Mwenyeezi Mungu ndiye Mwenye kushinda juu ya jambo lake, lakini watu wengi hawajui.

22. Na (Yusuf) alipofikilia utu uzima, tulimpa hukumu na elimu na hivyo ndivyo tunavyo walipa watendao mema.

23. Na (Mwanamke) ambaye nyumbani mwake (Yusuf) alikuwamo, akamtamani (Yusuf) kinyume cha nafsi yake, na akafunga milango, na akasema: Njoo, (Yusuf) akasema: Najikinga kwa Mwenyeezi Mungu, bila shaka yeye (mumeo) ni bwana wangu ametengeneza makazi yangu vizuri. Hakika madhalimu hawafaulu.

24. Na hakika (mwanamke huyo) akamkazia nia (ya kumtaka) na (Yusuf) akamkazia nia (ya kumkimbia) kama (Yusuf) asingeliona dalili ya Mola wake angelikaza nia kama alivyokaziwa yeye). Hivyo ndivyo ilivyotokea ili tumuepushie kila jambo la aibu na uovu. Hakika yeye alikua katika waja wetu waliosafishwa.

25. Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke huyo akairarua kanzu yake kwa nyuma, na wakamkuta mume wake mlangoni, mwanamke akasema: Hakuna malipo ya rnwenye kutaka ubaya kwa mkeo isipokuwa kufungwa gerezani au kupewa adhabu yenye kuumiza.

26 (Yusuf) akasema: Yeye amenitaka bila mimi kutaka. Na shahidi aliyekua katika jamaa za mwanamke akatoa ushahidi: Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele basi amesema kweli (mwanamke) naye (Yusuf) ni katika waongo.

27. Na kama kanzu yake imechanwa nyuma, basi amesema uongo (Mwanamke) naye (Yusuf) ni katika wakweli.

28. Basi (mumewe) alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma, akasema: Hakika hii ni katika hila zenu wanawake, bila shaka hila zenu ni kubwa.

29. Yusuf! yaachilie mbali haya, na wewe (mwanamke) omba msamaha kwa dhambi zako, hakika wewe ni miongoni mwa wakosaji.

30. Na wanawake wa mji ule wakasema: Mkewe mheshimiwa, anamtamani mtumishi wake kinyume cha nafsi yake. Hakika amemuathiri kwa mapenzi bila shaka sisi tunamuona yumo katika upotovu dhahiri.

31. Basi (mkewe mheshimiwa) aliposikia vitimbi vyao, akawaita na akawafanyia karamu na akampa kila mmoja wao kisu na akamwambia (Yusuf) tokea mbele yao. Basi walipomwona, wakamtukuza na wakakata mikono yao na wakasema: Hasha lillahi, huyu si mwanadamu, hakuwa huyu ila Malaika Mtukufu.

32. (Mkewe mheshimiwa) akasema: Huyu ndiye mliyenilaumia, na hakika nilimtamani kinyume cha nafsi yake, lakini akakataa. Na kama hatafanya ninayomwamuru lazima atafungwa gerezani na bila shaka atakuwa miongoni mwa madhalili.

33. (Yusuf) akasema: Ee Mola wangu! naipenda zaidi gereza kuliko haya wanayoniitia, na kama usiponiondoshea hila zao nitawaelekea na nitakuwa miongoni mwa wajinga.

34. Basi Mola wake akapokea maombi yake na akamuondoshea hila zao. Bila shaka yeye ndiye Mwenye kusikia, Mjuzi.

35. Kisha ikawadhihirikia baada ya kuona alama (kwamba) lazima wamfunge kwa muda kidogo.

36. Na wakaingia pamoia naye gerezani vijana wawili. Mmoja wao akascma: Hakika nimejiona (katika ndoto) nakamua ulevi. Na mwingine akasema: Hakika nimejiona (katika ndoto) nabeba mikate juu ya kichwa changu ambayo ndege wanaila. Tuambie tafsiri yake, hakika sisi tunakuona ni miongoni, mwa watu wazuri.

37. (Yusuf) akasema: Hakitakufikieni chakula mtakachopewa isipokuwa nitakuambieni hakika yake kabla hakijakufikieni. Hilo ni katika yale aliyonifundisha Mola wangu, hakika mimi nimeacha mila ya watu wasiomwamini Mwenyeezi Mungu, na wao hawaiamini Akhera.

38. Na nimefuata mila ya baba zangu Ibrahimu na Is’haqa na Yaakub, Haitufalii sisi kumshirikisha Mwenyeezi Mungu na chochote. Hivyo ni katika fadhili za Mwenyeezi Mungu zilizo juu yetu na juu ya watu wengine lakini watu wengi hawashukuru.

39. Enyi wafungwa wenzangu wawili, je waungu wengi wanaofarikiana ni bora au Mwenyeezi Mungu Mmoja, Mwenye nguvu?

40. Hamuabudu badala yake ila majina mlioyapanga wenyewe na baba zenu, Mwenyeezi Mungu hakuteremsha dalili kwa hayo. Haikuwa hukumu ila ni ya Mwenyeezi Mungu, ameamrisha msimuabudu isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui.

41. Enyi wafungwa wenzangu wawili! ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake pombe. Na ama mwingine (atauawawa kwa) kusulubiwa, na ndege watamla kichwa chake, limekatwa jambo mlilokuwa mkiuliza.

42. Na (Yusuf) akamwambia yule aliyemdhania kuwa ataokoka katika wawili hawa: Unikumbuke mbele ya bwana wako, Lakini shetani akamsahaulisha kumtaja kwa bwana wake, kwa hiyo (Yusuf) akakaa gerezani miaka michache.

43. Na mfalme akasema: Hakika mimi nimeona (katika ndoto) ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda, na mashuke saba mabichi na mengine yaliyokauka: Enyi wakubwa! Nambieni (maana ya) ndoto yangu ikiwa nyinyi mnaweza kufasiri ndoto.

44. Wakasema: Ni ndoto zilizovurugika wala sisi hatujui tafsiri ya ndoto.

45. Na akasema yule aliyeokoka katika wale (wafungwa) wawili na akakumbuka baada ya muda; Mimi nitakuambieni tafsiri yake basi nitumeni.

46. Yusuf ewe mkweli tueleze hakika ya ng’ombe saba wanene kuliwa na ng’ombe saba waliokonda, na mashuke saba mabichi na mengine yaliyokauka ili nirejee kwa watu wapate kujua.

47. Akasema: Mtalima miaka saba mfululizo kwa juhudi, na mtakavyovivuna basi viacheni katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mnavyokula.

48. Kisha itakuja baada ya hiyo miaka saba ya shida itakayokula vyote mlivyotanguliza, isipokuwa kidogo mtakachohifadhi.

49. Kisha baada ya hiyo utakuja mwaka mmoja ambao katika huo watu watasaidiwa na katika huo watakamua.

50. Na mfalme akasema: Mleteni kwangu basi (mjumbe wa mfalme) alipofika, (Yusuf) akasema: Rudi kwa bwana wako na ukamuulize imekuwaje shauri ya wanawake wale waliokata mikono yao bila shaka Mola wangu anazijua sana hila zao.

51. (Mfalme) akasema: Mlikuwa na kusudi gani mlipomtamani Yusuf kinyume cha matamanio yake? Wakasema: Hasha lillahi sisi hatukujua ubaya wowote kwake. Mkewe mheshimiwa akasema: Sasa haki imedhihirika, mimi ndiye nilimtamani kinyume cha nafsi yake, na bila shaka yeye ni miongoni mwa wakweli.

52. (NaYusuf akasema). Hayo ni kwa sababu mheshimiwa ajue kuwa mimi sikumfanyia khiyana nyuma yake, na kwamba Mwenyeezi Mungu haziongozi hila za makhaini.

53. Nami sijitakasi nafsi yangu, hakika nafsi ndiyo iamrishayo sana maovu isipokuwa yule ambaye Mola wangu amemrehemu, hakika Mola wangu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

54. Na mfalme akasema: Mleteni kwangu, nimchague awe mtu wangu mwenyewe. Basi alipozungumza naye, akasema: Hakika wewe leo kwetu ni mwenye heshima, mwenye kuaminika.

55. Akasema (Yusuf) niweke juu ya khazina za nchi, hakika mimi ndiye mlinzi, mjuzi.

56. Na hivyo ndivyo tulivyompa Yusuf cheo katika nchi, anakaa humo popote anapopenda. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye wala hatupotezi malipo ya wafayao mema.

57. Na bila shaka malipo ya Akhera ni bora zaidi kwa wale walioamini na wakawa wanamcha (Mwenyezi Mungu).

58. Na wakaja ndugu za Yusuf na wakaingia kwake, basi akawajua nao hawakumjua.

59. Na alipowapatia chakula chao, akasema: Nileteeni ndugu yenu aliyoko kwa baba yenu. Je, hamuoni kuwa mimi ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa wakaribishao?

60. Lakini msiponiletea, basi hampati kipimo chochote kwangu, wala msinikaribie.

61. Wakasema: Tutamshawishi baba yake na hakika sisi lazima tutafanya.

62. Na (Yusuf) akawaambia watumishi wake: Tieni bidhaa zao katika mizigo yao ili waione watakaporudi kwa watu wa nyumbani kwao, huenda watarejea.

63. Basi waliporejea kwa Baba yao, wakasema: Ewe Baba yetu! Tumenyimwa chakula basi mtume ndugu yetu pamoja nasi ili tupate kupimiwa, na kwa hakika sisi tutamlinda.

64. Akasema: Je, nikuaminini kwa huyu isipokuwa kama nilivyokuaminmi juu ya nduguye zamani. Basi Mwenyeezi Mungu ni mbora wa kulinda naye ndiye anayerehernu zaidi kuliko wenye kurehemu.

6o. Na walipofungua mizigo yao, wakakuta bidhaa zao wamerudishiwa, wakasema: Ewe baba yetu tunataka kingine nini? hii mali yetu imerudishwa kwetu! Na tutaleta chakula kwa ajili ya watu wetu, na tutamlinda ndugu yetu, na tutapata zaidi kipimo cha ngamia mmoja, hicho ni kipimo kidogo.

66. Akasema: Sitampeleka pamoja nanyi mpaka, mnipe ahadi kwa jina la Mwenyeezi Mungu kuwa lazima mtamleta kwangu, isipokuwa mzungukwe (na khatari) Basi walipompa ahadi yao akasema: Mwenyeezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa haya tusemayo.

67. Na akasema: Enyi wanangu! msiingie katika mlango mmoja bali ingieni katika milango mbali mbali, wala sikufaeni chochote mbele ya Mwenyeezi Mungu. Haiko hukumu ila kwa Mwenyeezi Mungu tu, kwake nimetegemea, basi wategemeao na wategemee kwake.

68. Na walipoingia jinsi alivyowaamrisha baba yao, haikuwafaa kitu kwa Mwenyeezi Mungu, isipokuwa haja iliyokuwa katika nafsi ya Yaakub aliitimiza. Na bila shaka yeye alikuwa Mwenye elimu kwa kuwa tulimfundisha, lakini watu wengi hawajui.

69. Na walipoingia kwa Yusuf akamkumbatia ndugu yake akasema: Hakika mimi .ni ndugu yako, basi usihuzunike kwa sababu ya yale waliyokuwa wakifanya.

70. Na alipokwisha wapatia chakula chao, akaweka kikopo cha kunywea maji katika mzigo wa nduguye, kisha mnadi akanadi: Enyi wasafiri! hakika nyinyi ni wezi.

71. Wakasema na hali ya kuwa wamewaelekea mmepoteza nini?

72. Wakasema: Tumepoteza kopo la mfalme na atakayelileta atapewa mzigo wa ngamia, mimi ni mdhamini wake.

73. Wakasema: Wallahi! mmekwisha jua ya kuwa sisi hatukuja kufanya uharibifu katika nchi, wala sisi si wezi.

74. Wakasema: Basi malipo yake yatakuwa nini kama nyinyi ni waongo?

75. Wakasema: malipo yake ni yule ambaye itaonekana katika mzigo wake, basi yeye ndiye malipo yake! hivyo ndivyo tunavyo walipa madlialimu.

76. Basi akaanza (Yusuf) na mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye, kisha akakitoa katika mzigo wa nduguye. Hivyo ndivyo tulivyomfanyia hila Yusuf, hakuweza kumzuia nduguye kwa kanuni ya mfalme, isipokuwa alivyotaka Mwenyeezi Mungu tunamwinua vyeo yule tunayemtaka, na juu ya kila mwenye elimu yuko ajuaye zaidi.

77. Wakasema: Kama ameiba, basi ndugu yake pia aliiba zamani lakini Yusuf akayaweka siri moyoni mwake, wala hakuwadhihirishia. Akasema: Nyinyi mna hali mbaya, na Mwenyeezi Mungu anajua mnayoyasema.

78. Wakasema: Ewe mheshimiwa! hakika anaye baba mzee sana, kwa hiyo shika mmoja wetu badala yake, hakika sisi tunakuona ni miongoni mwa wenye hisani.

79. (Yusuf) akasema: Mwenyeezi Mungu apishe mbali kumshika (yeyote) ila yule tuliyekuta mali yetu iko kwake, tusije kuwa madhalimu.

80. Basi walipomkatia tamaa, wakaenda kando, kunong’ona. Mkubwa wao akasema: Je, hamjui kuwa baba yenu amechukua ahadi juu yenu kwa jina la Mwenyeezi Mungu, na zamani pia mlikosa katika (tukio la) Yusuf? Basi sitatoka nchi hii mpaka baba yangu aniruhusu au Mwenyeezi Mungu anihukumu, naye ni mbora wa mahakimu.

81. Rudini kwa baba yenu, na semeni! Ewe baba yetu! hakika mwanao ameiba, na sisi hatukushuhudia isipokuwa yale tuliyoyajua, na hatukuwa wenye kulinda yaliyokuwa katika siri.

82. Na waulize watu wa mji tuliokuwa na msafara tuliofika nao, na hakika sisi tunasema kweli.

83. (Yaakub) akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini jambo fulani, lakini subira ni njema huenda Mwenyeezi Mungu akaniletea wote pamoja, kwani yeye ni Mjuzi, Mwenye hekima.

84. Na akajitenga nao, na akasema: Oh majonzi yangu juu ya Yusuf! na macho yake yakawa meupe kwa huzuni, aliyokuwa akiizuia.

85. Wakasema: Wallahi, hutaacha kumkumbuka Yusuf hata utakuwa mgonjwa au utakuwa miongoni mwa wenye kuangamia.

86. Akasema; Hakika mimi nashtakia masikitiko yangu na huzuni yangu kwa Mwenyeezi Mungu, na ninajua kwa Mwenyeezi Mungu msiyoyaiua.

87. Enyi wanangu! nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa katika rehema ya Mwenyeezi Mungu. Hakika hakati tamaa ya rehema ya Mwenyeezi Mungu isipokuwa watu makafiri.

88. Basi walipoingia kwa (Yusuf) wakasema: Ewe mheshimiwa! shida imetupata sisi na watu wetu, na tumeleta bidhaa isiyotakiwa, kwa hiyo tupimie kipimo kamili na (fanya kama) unatupatia sadaka. Hakika Mwenyeczi Mungu huwalipa wanaofadhili.

89. Akasema je, mnajua mliyomfanyiaYusuf na nduguye mlipokuwa wajinga?

90. Wakasema: Je, hakika wewe ndiye Yusuf akasema: Mimi ndiye Yusuf na huyu ni ndugu yangu. Bila shaka Mwenyeezi Mungu ametufanyia hisani kwani anayemcha (Mwenyeezi Mungu) na kusibiri, basi hakika Mwenyeezi Mungu hapotezi malipo ya wafanyao mema.

91. Wakasema: Wallahi bila shaka Mwenyeezi Mungu amekufadhilisha kuliko sisi na hakika sisi tulikuwa wenye makosa.

92. Akasema (Yusuf): Hakuna lawama juu yenu leo, Mwenyeezi Mungu atakusameheni, naye ni Mwenye rehema zaidi kuliko wanaorehemu.

93. Nendeni na kanzu yangu hii na mumwekee usoni baba yangu, atakuwa mwenye kuona. Na mniletee watu wenu wote wa nyumbani.

94. Na ulipoondoka msafara (katika Misri) baba yao akasema hakika napata harufu ya Yusuf ikiwa hamtaniona zuzu.

95. Wakasema: Wallahi hakika ungali katika upotovu wako wa zamani.

96. Basi alipofika mtoaji wa khabari njema, akaiweka (kanzu ya Yusuf) mbele ya uso wake, mara aliona akasema je, sikuwaambieni, hakika mimi najua kwa Mwenyeezi Mungu msiyoyajua?

97. Wakasema: Ewe baba yetu! tuombee msamaha kwa dhambi zetu, hakika sisi tulikuwa wenye makosa.

98. Akasema: Nitakuombeeni msamaha kwa Mola wangu, kwani yeye ndiye Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.

99. Na walipoingia kwa Yusuf akawakumbatia wazazi wake na akasema: Ingieni Misri, Inshaallah kwa amani.

100. Na akawanyanyua wazazi wake na kuwaweka katika kiti chake na wote wakaporomoka kumsujudia (Mwenyeezi Mungu) na akasema: Ewe baba yangu! hii ndiyo tafsiri ya ndoto yangu ya zamani. Bila shaka Mola wangu amehakikisha, na amenifanyia hisani aliponitoa gerezani na kuwaleteni nyinyi kutoka Jangwani baada ya shetani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu ni Mpole kwa amtakaye kwani yeye ni Mjuzi, Mwenye hekima.

101. Ee Mola wangu! hakika umenipa utawala na umenifundisha tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera, nifishe hali ya kuwa ni Mwislaamu na nichanganye na watendao mema.

102. Hizo ni katika khabari za siri tulizo kufunulia, na hukuwa pamoia nao walipoazimia shauri lao hali wakifanya hila.

103. Na wengi katika watu hawatakuwa wenye kuamini hata ukijitahidi vipi.

104. Wala huwaombi malipo juu ya haya hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu.

105. Na dalili ngapi katika mbingu na ardhi wanazozipitia, na hali yakuwa wanazipuuza.

106. Na wengi wao hawamwamini Mwenyeezi Mungu isipokuwa wao ni washirikina tu.

107. Je, wanajiona salama kuwa hautawafikia (msiba wa) adhabu ya Mwenyeezi Mungu au kuwaflkia Kiyama kwa ghafla na hali hawatambui?

108. Sema: Hii ndiyo njia yangu, ninalingania kwa Mwenyeezi Mungu kwa ujuzi, mimi na wanaonifuata, na Mwenyeezi Mungu ametakasika na kila upungufu wala mimi simo miongoni mwa washirikina.

109. Na hatukupeleka (Mtume) kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia Wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Je hawakutembea katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wale wamchaoJe, hamfahamu?

110. Hata Mtume walipokata tamaa (na makafiri) wakaona kuwa wamekadhibishwa, msaada wetu ukawafikia, basi akaokolewa tuliyemtaka, na haiondolewi adhabu yetu kwa watu waovu.

111. Bila shaka katika hadithi zao limo fundisho kwa wenye akili. Si maneno yaliyozushwa, bali ni ya kusadikisha yaliyokuwa kabla yake, na ni maelezo ya kila kitu, na ni mwongozo na rehema kwa watu wenye kuamini.