Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 8
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Naapa kwa Tiini na Zaytun.
2. Na kwa mlima Sinai.
3. Na kwa mji huu wenye amani.
4. Bila shaka tumemuumba mtu katika hali nzuri sana.
5. Kisha tukamrejesha chini ya walio chini.
6. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema basi watapata malipo mema yasiyokoma.
7. Basi ni nani atakayekukadhibisha baada ya haya katika hukumu.
8. Je, Mwenyeezi Mungu si Hakimu bora kuliko Mahakim (wote)?