Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 8
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Kumewashughulisha mno kutaka wingi (wa mali).
2. Mpaka mmeingia makaburini.
3. Sivyo, karibuni mtajua.
4. Kisha hapana, hivi karibuni mtajua.
5. Sivyo, lau mngelijua kwa elimu ya yakini.
6. Hakika mtauona Moto!
7. Kisha mtauona kwa jicho la yakini.
8. Kisha mtaulizwa siku hiyo neema zote.