Surah Shams

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 15

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Naapa kwa jua na mwanga wake.

2. Na kwa mwezi unapoliandama.

3. Na kwa mchana unapolidhihirisha.

4. Na kwa usiku unapolifunika.

5. Na kwa mbingu na kwa yule aliyeijenga.

6. Na kwa ardhi na kwa yule aliyeitandaza.

7. Na kwa nafsi na kwa yule aliyeitengeneza.

8. Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake.

9. Bila shaka amefaulu aliyeitakasa.

10. Na bila shaka amepata khasara mwenye kuitweza.

11. Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotovu.

12. Aliposimama muovu wao mkubwa.

13. Hapo Mtume wa Mwenyeezi Mungu akawaambia: (Huyu) ni ngamia wa Mwenyeezi Mungu (tahadharini naye) na kinywaji chake.

14. Lakini walimkadhibisha na wakamchinja. Kwa hiyo Mola wao aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao, na akifanya sawa.

15. Wala haogopi matokeo yake.