Surah Quraish

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 4

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Kwa ajili ya Makuraishi kuzowea.

2. Kuzowea safari ya kusi na kaskazi.

3. Basi wamuabudu Mola wa nyumba hii.

4. Ambaye amewalisha wakati wa njaa na amewapa amani wakati wa khofu.