Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 11
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Kiyama
2. Ni nini Kiyama?
3. Na nini kitakujulisha ni nini Kiyama?
4. Siku ambayo watu watakuwa kama panzi waliotawanywa.
5. Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa.
6. Basi ama yule mizani yake itakuwa nzito.
7. Basi yeye atakuwa katika maisha yanayopendeza.
8. Na ama yule ambaye mizani yake itakuwa nyepesi.
9. Basi makazi yake yatakuwa Motoni.
10. Na nini kitakujulisha Haawiya ni nini?
11. Ni Moto mkali mno.