Surah Nasr

Sura hii imeteremshwa Madina, na ina Aya 3

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1.  Utakapofika msaada wa Mwenyeezi Mungu na ushindi.

2.Na utawaona watu wakiingia dini ya Mwenyeezi Mungu makundi makundi.

3. Basi mtakase Mola wako kwa sifa njema na umuombe msamaha, hakika yeye ndiye apokeaye sana toba.