Sura bii imeteremshwa Makka, na ina Aya 40
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Wanaulizanakhabari gani?
2. Khabari iliyo kuu.
3. Ambayo wanakhitilafiana.
4. Siyo, hivi karibuni watajua.
5. Tena siyo, hivi karibuni watajua.
6. Je, hatukuifanya ardhi kuwa tandiko
7. Na milima (kama’) vigingi.
8. Na tukakuumbeni wanaume na wanawake.
9. Na tukaufanya usingizi wenu kama kufa.
10. Na tukaufanya usiku (kama) vazi.
11. Na tukaufanya mchana. (kama) kufufuka.
12. Na tukajenga juu yenu (mbingu) saba madhubuti.
1 3. Na tukaifanya taa ing’aayo na yenye joto sana.
14. Na tukateremsha maji yaangukayo kwa kasi kutoka mawinguni.
15. Ili kwayo tuoteshe nafaka na mimea.
16. Na mabustani yenye miti iliyofunga.
17. Kwa hakika siku ya hukumu imewekewa wakati maalumu.
18. Siku itakapopigwa baragumu nanyi mtafika makundi makundi.
19. Na mbingu zitafunguliwa ziwe milango milango.
20. Na milima itaondolewa na itakuwa kama maji (ukiona kwa mbali).
21. Kwa hakika Jahannam inangoja.
22. Ni makazi ya waasi.
23. Wakae humo milele.
24. Hawataonja humo baridi wala kinywaji.
25. Ila maji yachemkayo sana na usaha.
26. (Watalipwa) malipo sawa sawa.
27. Hakika wao hawakutumai (kama itakuwako) hesabu.
28. Na wakakadhibisha Aya zetu kukadhibisha (kukubwa).
29. Na kila kitu tumekidhibiti kwa maandiko.
30. Basi onjeni nasi hatutakuzidishieni ila adhabu.
31. Bila shaka wamchao (Mwenyeezi Mungu) wamewekewa kufuzu.
32. Mabustani na mizabibu.
33. Na wanawari walio umri mmoja.
34. Na vikombe vilivyojaa.
35. Hawatasikia humo maneno ya upuuzi wala kukadhibisha.
36, Watalipwa kutoka kwa Mola wako kipawa kilichohesabiwa.
37. Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake, Mwingi wa rehema, hawataweza kusema naye.
38. Siku ambayo atasimama Roho (Jibril) na Malaika safu safu, hawatazungumza ila ambaye Mwenyeezi Mungu Mwingi wa rehema amempa idhini, na atasema yaliyosawa.
39. Hiyo ndiyo siku ya haki, basi anayetaka ashike makao kwa Mola wake.
40. Hakika tunakuhadharisheni adhabu iliyo karibu, siku ambayo mtu atayaona iliyoyatanguliza mikono yake miwili, na kafiri atasema: Laiti ningelikuwa udongo.