Surah Maa’un

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 7

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Je unamjua ambaye anakadhibisha dini?

2. Huyo ndiye anaye msukuma yatima.

3. Wala hahimizi kumlisha masikini.

4. Basi ole wao wanaoswali.

5. Ambao wanapuuza swala zao.

6. Ambao wao hujionyesha.

7. Wakazuilia (watu) manufaa.