Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 5
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Imeangamia mikono miwili ya Abu Lahab naye ameangamia.
2. Hayatamfaa mali yake wala alichokichuma.
3. Hivi karibuni ataingia katika Moto wenye muwako.
4. Na mkewe, mchukuzi wa kuni.
5. Shingoni mwake mna kamba iliyosokotwa.