Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 6
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Sema: Enyi makafiri.
2. Siabudu mnachoabudu.
3. Wala nyinyi hamuabudu ninayemwabudu.
4. Wala sitaabudu mnachoabudu.
5. Wala nyinyi hamtaabudu ninayemwabudu.
6. Nyinyi mtapata malipo yenu nami nitapata malipo yangu.