Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 8
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1.Je, hatukukupanulia kifua chako?
2.Na tukakuondolea mzigo wako.
3.Ambao ulielemea mgongo wako.
4.Na tukakutukuzia sifa zako.
5.Basi kwa hakika pamoja na dhiki iko faraja.
6.Hakika pamoja na dhiki iko faraja.
7.Basi ukipata faragha, fanya juhudi.
8.Na kwa Mola wako elekea kwa shauku.