Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 4
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Sema: Yeye Mwenyeezi Mungu ni Mmoja.
2. Mwenyeezi Mungu ndiye anayekusudiwa kwa haja.
3. Hakuzaa wala hakuzaliwa.
4. Wala hana anayefanana naye hata mmoja.