Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 9
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Ole wake kila safihi, msengenyaji.
2. Ambaye amekusanya mali na kuyahesabu.
3. Anadhani kuwa mali yake yatambakisha milele.
4. Sivyo, lazima atatupwa katika Hutama!
5. Na nini kitakujulisha ni nini Hutama.
6. Ni Moto wa Mwenyeezi Mungu uliowashwa.
7. Ambao unapanda nyoyoni.
8.Hakika huo (Moto) utafungwa juu yao.
9. Ndani ya nguzo ndefu ndefu.