Surah Hijr

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 99

 Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

1. Alif Lam Ra. Hizo ni Aya za Kitabu na za Qur’an yenye kuweka wazi.

2. Huenda wale waliokufuru wanapenda wangelikuwa Waislamu.

3. Waache wale (chakula) na wastarehe, na liwadanganye tumaini la uwongo, karibuni watajua.

4. Na hatukuuangamiza mji wowote ila ulikuwa na hukumu maalumu.

5. Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala hawawezi kukawiza.

6. Na wakasema: Ewe uliyeteremshiwa mawaidha hakika wewe ni rnwehu.

7. Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli?

8. Sisi hatuteremshi Malaika ila kwa haki na hapo hawatapewa muda.

9. Hakika sisi tumeiteremsha Qur’an, na hakika sisi ndio wenye kuilinda.

10. Na bila shaka tulikwisha waleta (Mitume) kabla yako katika makundi ya (watu) wa kwanza.

11. Na hakuwafikia Mtume yeyote isipokuwa walimfanyia mzaha.

12. Hivyo ndivyo tunavyoiingiza (tabia ya mzaha) katika nyoyo za waovu.

13. Hawayaamini na hali umekwisha pita mfano wa (watu) wa kwanza.

14. Na lau tungeliwafungulia mlango wa mbingu, na wakawa wanapanda (humo).

15. Lazima wangelisema: Macho yetu yamelewalewa tu, bali sisi ni watu tuliorogwa.

16. Na kwa hakika tumeweka katika mbingu vituo (vya nyota) na tumezipamba kwa ajili ya watazamao.

17. Na tumezilinda na kila shetani afukuzwaye.

18. Lakini asikilizaye kwa wizi, mara humfuata kijinga king’aacho.

19. Na ardhi tumeitandaza na humo tumeweka milima na tumeotesha humo kila kitu kwa kiasi chake.

20. Na tumekufanyieni humo vitu vya maisha, na ya yule nyinyi hamumpi riziki.

21. Na hakuna chochote ila tunayo khazina yake, wala hatukiteremshi isipokuwa kwa kipiino maalumu.

22. Na tunazipeleka pepo zimejaa umande na tunateremsha maji kutoka mawinguni, kisha tunakunywesheni hayo, wala si nyinyi muyawekayo akiba.

23. Na kwa hakika sisi ndio tuhuishao na tufishao, na sisi ndio warithi.

24. Na hakika tunawajua watanguliao katika nyinyi, na hakika tunawajua wachelewao.

25. Na bila shaka Mola wako yeye ndiye atawakusanya, kwani yeye ni Mwenye hekima, Mjuzi.

26. Na bila shaka tulimuumba mwanadamu kwa udongo mkavu utoao sauti, unaotokana na matope meusi yaliyovunda.

27. Na majinni tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo wenye joto.

28, Na (kumbuka) Mola wako alipowaambia Malaika: Hakika mimi nitamuumba mtu kwa udongo mkavu utoao sauti, unaotokana na matope meusi yaliyovunda.

29. Basi nitakapomkamilisha na kumpulizia roho yangu, basi mumuangukie kwa kumtii.

30. Basi Malaika wakatii wote pamoja.

31. Isipokuwa Iblis, akakataa kuwa pamoia na waliotii.

32. (Mwenyeezi Mungu) akasema: Ewe iblis! umekuwaje hukuwa pamoja na waliotii?

33. Akasema: Siwezi kumtii mtu uliyemuumba kwa udongo mkavu utoao sauti unaotokana na matope meusi yaliyovunda.

34 Akasema (Mwenyeezi Mungu): Basi toka humo, maana hakika wewe ni mwenye kufukuzwa.

35. Na kwa hakika itakuwa juu yako laana mpaka siku ya hukumu.

36. Akasema (Iblis): Mola wangu! basi nipe nafasi mpaka siku watakayofufuliwa.

37. Akasema (Mwenyeezi Mungu). Hakika wewe ni katika wale waliopewa nafasi.

38. Mpaka siku ya wakati uliowekwa.

39. Akasema (Iblis) Molawangu! kwa sababu umenihukumu kupotea, lazima nitawapambia (upotovu) katika ardhi na nitawapoteza wote.

40. Isipokuwa waja wako miongoni mwao waliosafishwa.

41. (Mwenyeezi Mungu) akasema: Hii ndiyo njia (yao) ya (kuja) kwangu imenyooka.

42. Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipokuwa yule mwenye kukufuata katika wapotovu.

43. Na hakika Jahannam ndipo mahala pao walipoahidiwa wote.

44. Ina milango saba, kwa kila mlango iko sehemu yao iliyogawanywa.

45. Hakika wamchao (Mwenyeezi Mungu) watakuwa katika mabustani na chemchem.

46. Yaingieni kwa salama (na) amani.

47. Na tutaondoa. mfundo uliomo vifuani mwao, na (watakuwa) ndugu wakikaa juu ya viti (vya kifalrne) kwa kuelekeana.

48. Haitawagusa humo taabu, wala humo hawatatolewa.

49. Waambie waja wangu kwamba: Mimi ni Mwingi wa kusarnehe, Mwenye kurehemu.

50. Na hakika adhabu yangu ni adhabu yenye kuumiza.

51. Na uwaambie khabari za wageni wa Ibrahimu.

52. Walipoingia kwake na wakasema: Salama. Akasema: kwa hakika sisi tunakuogopeni.

53. Wakasema: Usiogope, kwa hakika sisi tunakupa khabari njema ya mtoto mwenye elimu.

54. Akasema: Je mnanipa khabari njema hali uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanipa khabri njema?

55. Wakasema: Tumekupa khabari njema iliyo haki, basi usiwe miongoni mwa wakatao tamaa.

56. Akasema: Na nani anayekata tamaa ya rehema ya Mola wake isipokuwa wale waliopotea?

57. Akasema tena kusudi lenu ni nini enyi mliotumwa?

58, Wakaserna: Hakika sisi tumetumwa kwa watu waovu.

59. Isipokuwa waliomfuata Luti, bila shaka sisi tutawaokoa wote.

60. Ila mkewe, tunapimia kuwa atakuwa miongoni rnwa wakaao nyuma.

61. Basi wajumbe walipofika kwa watu wa Luti.

62. Akasema: Hakika nyinyi ni watu msiojulikana.

63. Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale ambayo walikuwa wanayafanyia shaka.

64. Na tumefika kwako kwa haki, na hakika sisi ni wasemao kweli.

65. Basi ondoka na watu wako katika kipande cha usiku, na wewe ufuate nyuma yao, wala yeyote katika nyinyi asigeuke nyuma na mwende mnakoamrishwa.

66. Na tukamkatia hukumu hiyo, ya kwamba (hata) wa mwisho (wao) hao (ikifika) asubuhi atakuwa amekatiliwa mbali.

67. Na wakaja watu wa mji wakifurahi.

68. Akasema: Hakika hawa ni wageni wangu kwa hiyo msinifedheshe.

39. Na muogopeni Mwenyeezi Mungu wala msinidhalilishe.

70. Wakasema: Je, sisi hatukukataza (kukaribisha) watu (wa nje?)

71. Akasema: Hawa ni binti zangu ikiwa nyinyi ni wafanyao.

72. Kwa kiapo cha maisha yako, hakika wao katika ulevi wao wanahangaika.

73, Mara adhabu ikawakamata lilipotoka jua.

74. Basi tukaufanya (mji ule) juu yake kuwa chini yake, na tukawapigishia mvua ya mawe ya udongo.

75. Hakika katika hayo yamo mazingatio kwa watu wenye busara.

76. Na (mji) huo upo kwenye barabara ipitwayo.

77. Bila shaka katika hayo yarno mazingatio kwa Waumini.

78. Na hakika watu wa kichaka (pia) walikuwa madhalimu.

79. Kwa hiyo tukawaadhibu, na (miji) hiyo miwili iko kwenye barabara iliyo wazi.

80. Na bila shaka wakazi wa (mji wa) Hijri (pia) waliwakadhibisha Mitume.

81. Na tuliwapa maonyo yetu, lakini walikuwa wakiyapuuza.

82. Nao walikuwa wakichonga majumba katika majabali kwa amani.

83. Basi ukelele ukawachukua asubuhi.

84. Na hayakuwafaaa waliyokuwa wakiyachuma.

85. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yao ila kwa haki, na bila shaka Kiyama kitafika, basi samehe msamaha mzuri.

86. Hakika Mola wako ndiye Muumbaji Mjuzi.

87. Na kwa hakika tumekupa (Aya) saba zisomwazo rnara kwa mara na Qur’an tukufu.

88. Usikodolee macho yako yale tuliyowastareheshea makundi mbali mbali kati yao, wala usiwahuzunikie, na inamisha bawa lako kwa waumini.

89. Na sema: Hakika mimi ni Muonyaji niliyedhahiri.

90. Kama tulivyowateremshia waliojigawanya makundi.

91. Ambao wameifanya Qur’an vipande vipande.

92. Na kwa haki ya Mola wako lazima sisi tutawauliza wote.

93. Juu ya yale waliyokuwa wakiyatenda.

94. Basi yatangaze uliyoamrishwa na ujitenge mbali na washirikina.

95. Hakika sisi tunakutosha kwa (shari ya) wafanyao dhihaka.

96. Ambao wanaofanya kuwa pamoja na Mwenyeezi Mungu, mungu mwingine basi karibuni watajua.

97. Na kwa hakika Sisi tunajua kuwa kifua chako kinadhikika kwa yale wanayosema.

98. Basi mtukuze Mola wako kwa sifa njema, na uwe miongoni mwa wanaosujudu.

99. Na umwabudu Mola wako mpaka yakufikie mauti.