Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 26
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Je, imekufikia khabari ya Kiyama?
2.Siku hiyo nyuso zitakuwa na huzuni.
3.Zitatumika na kutaabika.
4.Zitaingia katika Moto mkali.
5. Watanyweshwa katika chemchem ichemkayo.
6.Hawatakuwa na chakula isipokuwa cha miba.
7. Hakinenepeshi wala hakifai kwa njaa.
8. Nyuso siku hiyo zitanawiri.
9.Watakuwa radhi kwa amali yake.
10.Katika Bustani tukufu.
11.Humo hutasikia upuuzi.
12. Humo mna chemchem inayotiririka.
13.Humo mna viti vya fakhari.
14.Na vikombe vilivyowekwa.
15.Na mito iliyopangwa.
16.Na ma^ulia yaliyotandikwa.
17. Je, hawamtazami ngamia namna gani alivyoumbwa.
18.Na mbingu namna gani zilivyoinuliwa?
19.Na milima jinsi ilivyosimikwa?
20.Na ardhi jinsi ilivyotandazwa?
21. Basi kumbusha hakika wewe ni Mkumbushaji tu.
22. Wewe si mwenye kuwatawalia.
23.Lakini anayerudi nyuma na kukataa.
24. Mwenyeezi Mungu atamuadhibu adhabu kubwa sana.
25. Hakika marejeo yao ni kwetu.
26. Kisha bila shaka hesabu yao ni juu yetu.