Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 5
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Je, hukuona jinsi Mola wako alivyowafanya wenye tembo?
2. Je, hakuiharibu hila yao?
3. Na akawapelekea juu yao ndege makundi makundi?
4. Wakawatupia mawe ya udongo mkavu.
5. Na akawafanya kama majani yaliyoliwa.