Surah Dhuha

Sura hii irneterernshwa Makka, na ina Aya 11

Kwajina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Naapa kwa mwanzo wa mchana.

2. Na kwa usiku unapotanda.

3. Hakukuacha Mola wako wala hakukasirika.

4. Na bila shaka mwisho ni bora kwako kuliko mwanzo.

5. Na Mola wako hivi karibuni atakupa na utaridhika.

6. Je, hakukukuta ni yatima akakuhifadhi?

7. Na akakukuta ukihangaika (kuongoza watu) naye amekuongoza?

8. Na akakukuta mhitaji naye amekutajirisha.

9. Basi usimkemee yatima.

10. Wala mwenye kuomba usimkaripie.

11. Na neema ya Mola wako izungumze.