Surah Balad

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 20

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Naapa kwa mji huu.

2. Na wewe utashuka katika mji huu.

3. Naapa kwa mzazi na alichokizaa.

4. Hakika tumemuumba mwanadamu katika taabu.

5. Je anadhani kuwa hapana yeyote mwenye uwezo juu yake?

6. Anasema: Nimeharibu mali nyingi (bure).

7. Je, anadhani kuwa hapana yeyote anayemuona?

8. Je, hatukumpa macho mawili?

9. Na ulimi, na midomo miwili.

10. Na tukamuongoza njia mbili.

11. Lakini hakupita njia nzito.

12. Na nini kitakujulisha njia nzito ni nini!

13. Ni kumwacha huru mtumwa.

14. Au kumlisha siku ya njaa.

15. Yatima aliye jamaa.

16. Au masikini mwenye haja.

17. Kisha awe miongoni mwa waumini na wanaousiana kusubiri na wanaousiana kuhurumiana.

18. Hao ndio watu wa kheri.

19. Na waliokataa Aya zetu, hao ndio watu wa shari.

20. Moto uliofungwa uko juu yao.