Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 19
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
1. Litakase jina la Mola wako aliye Mtukufu.
2. Ambaye ameumba akakamilisha.
3. Na ambaye amekadiria na akaongoza.
4. Na ambaye ameotesha malisho.
5. Kisha akayafanya makavu, yenye kupiga weusi.
6. Tutakusomesha wala hutasahau.
7. Ila akipenda Mwenyeezi Mungu, hakika yeye anayajua yaliyo wazi na yaliyofichika.
8. Na tutakurahisishia yawe mepesi.
9. Basi kumbusha ikiwa utafaa ukumbusho.
10. Atakumbuka anayemcha (Mwenyeezi Mungu).
11. Na atajiepusha nao mwingi wa mateso.
12. Ambaye atauingia Moto mkubwa.
13. Kisha humo hatakufa wala hatakuwa hai.
14. Hakika amekwisha faulu aliyejitakasa.
15. Na akakumbuka jina la Mola wake na akaswali.
16. Lakini nyinyi mnapenda zaidi maisha ya dunia.
17. Hali akhera ni bora na yenye kudumu.
18. Hakika haya yamo katika Vitabu vya kwanza.
19. Vitabu vya Ibrahimu, na Musa.