Surah Aadiyaat

Sura hii imeteremshwa Makka, na ina Aya 11

Kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

1. Naapa kwa farasi wanaokwenda mbio wakitweta.

2. Wanaotoa moto kwa kupiga kwato.

3. Tena kwa wale wanaoshambulia wakati wa asubuhi.

4. Wakarusha mavumbi wakati huo.

5- Wakaingia katikati ya kundi.

6. Hakika Mwanadamu ni mtovu wa shukrani sana kwa Mola wake.

7. Naye hasa ni shahidi wa hayo.

8. Naye kwa hakika ana mapenzi sana na mali.

9.Je, hajui watakapofufuliwa waliomo makaburini!

10. Na yakadhihirishwa yaliyomo vifuani!

11. Hakika Mola wao atawajua sana siku hiyo.